Baada ya kuweka headlines nyingi na movie ya ‘Straight Outta Compton’, Dr. Dre amekuwa akifikiria vitu vingi sana, je Dr. Dre ana mipango gani kimuziki sasa hivi? Kama wewe ni shabiki wa producer huyo basi hii taarifa ikufikie popote pale ulipo…
Kwenye kipindi chake cha The Pharmacy kinachoruka kupitia Beats 1 Radio, Dr. Dre alipata time ya kufanya interview na rapper Snoop Dogg na kumuelezea mawazo yake machache kuhusiana na kurudi jukwani na Snoop Dogg mwenyewe, Eminem pamoja na Kendrick Lamar, na kwenye safari yake yote ya muziki Dr. Dre anadai hajawahi kufanya tour kubwa Europe!
Dr. Dre.
Licha ya yeye kuwa na nia hiyo, safari hii producer huyo amesema angependa kuonyesha upendo kwa mashabiki wake wa Europe kwa kufanya tour hiyo na mastaa watatu wakubwa katika game ya muziki wa HipHop na kuperform nao huko kwenye jukwaa moja…
>>> “nataka
niite hiyo tour ‘Beats & Rhymes’. Nataka niwepo mimi, wewe, nataka
pia awepo Eminem na Kendrick Lamar… yeah ningependa kufanya tour Europe
nzima na kuiita Beats & Rhymes, kuchukua coverage na production ya
tour nzima kutoka hapa mpaka huko na kuwaonyesha mashabiki wangu wa
Europe upendo wa kipekee sana kwa sababu wamekuwa na mimi kwa miaka
mingi na upendo wao umekuwa wa kipekee sana kwangu kwenye safari yangu
ya muziki… So hiyo ndio ndoto yangu kwa sasa. Natumaini tutaifanikisha.” <<< Dr. Dre.
Snoop Dogg.
Wakati Dr. Dre anaongea yote haya, Snoop Dogg alionekana kumuunga mkono producer huyo bila kipingamizi… na pia kutoa wazo la jina lingine la tour hiyo…
>>> ” Hiyo ndoto imekaa vizuri… mimi ningeshauri tuiite ‘Hoodstock’ au vipi?” <<< alisema Snoop Dogg.
0 comments:
Post a Comment