Thursday, 22 October 2015

Collabo ya D’Banj na jamaa wa TZ.. Video ya ‘Aiyola’ imekamilika?

Leave a Comment
Kuna mkali mwingine ambaye ni underground kutoka Shinyanga TZ kaingia kwenye headlines kubwa baada ya kufanikiwa kupata connection ya kufanya ngoma na mkali toka Nigeria, D’Banj.
Jamaa hana jina kubwa kwenye Bongo Fleva lakini amesimulia jinsi ambavyo aliweza kuingia kwenye ukurasa wa D’Banj wa Instagram na kufanikiwa kushiriki Shindano la kuandaa wimbo ambao jamaa aliupenda na kumkubalia kufanya nae wimbo.
Mkali mwingine ambaye anatoka lebo ya Wasafi Classic ambayo iko chini ya Diamond Platnumz, Harmonize tayari Bongo Fleva imempokea kwa mikono miwili baada ya kuachia ngoma ya ‘Aiyola‘, vipi mipango ya Video je?
Jamaa amesema siku kadhaa hivi zilizopita alifanikiwa kusafiri na kutua Soutth Africa kwa ajili ya kushoot Video yake… kazi imekamilika na tuijarajie wakati wowote hewani mtu wangu.
Budget ya video je? Harmonize amesema gharama imekuwa kubwa kwa sababu waliamua kuweka pesa ya kutosha ili kitu kitokee poa kama ambavyo watu wameipokea poa audio ya wimbo wake.
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: