Saturday, 24 October 2015

Siasa Dakika nne za Mchekeshaji Kingwendu na mipango yake Ubunge wa Kisarawe..

Leave a Comment
Muigizaji Kingwendu ni miongoni mwa mastaa ambao wamechukua headline za kugombea Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kama Afande Sele, Professor Jay, Muigizaji Frank na wengine.
Mchekeshaji na muigizaji Kingwendu anagombea ubunge kwenye jimbo la Kisarawe mkoa wa Pwani kupitia tiketi ya CUF, Kingwendu hakuwahi kusikika kabisa tangu kampeni zianze, lakini kabla October 20 2015 Jumapili haijafika leo amekaa na sisi kwenye exclusive na millardayo.com na kutupa mipango yake kwenye Siasa inavyokwenda.
Tangu kampeni zianze huku hali ni nzuri na nina faida kubwa ya kushinda sasa hivi Wazaramo wameamka wanataka mabadiliko, muda mrefu wamewapa umaskini wamewadharirisha na wamewanyima elimu lakini mimi huku nimewafufua vizuri wamenielewa na mikakati yangu… watu wamenielewa vizuri na wako tayari kupiga kura kwa Kingwendu’- Kingwendu.
wwwwwwwwwww
Nitakapoingia Bungeni sitofanya kazi ya uchekeshaji, kazi iliyonileta bungeni ni kutetea wananchi, kuwaletea maendeleo na kufuta kero zote za wananchi… si vyema tena kuingia kwenye majukwaa na kukata viuno kwa kuwa tayari nitakuwa Mheshimiwa
Kwenye sentensi nyingine Kingwendu ameyaongea haya >>> “Nitakapokuwa Bungeni nitaepukana na ile sauti niliyokuwa naitumia katika sanaa nitakuwa na sauti ya kawaida, nitajenga hoja za Msingi ninataka kutoa mfano kwa viongozi waliopita Kisarawe habari ndio hiyo“- Kingwendu.
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: