October 22 2015 ni wiki ya tatu zimepita tangu aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Democratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila afariki kwa ajali ya gari ndogo eneo la Msolwa, Chalinze Mkoa wa Pwani.
Rais JK akimpa pole Mama Georgia Mtikila siku mwili wa Marehemu Mtikila ulipoagwa Viwanja vya Karimjee Dar.
Mama Georgia Mtikila ni mke wa Marehemu Mchungaji Mtikila… leo kwa mara ya kwanza amekutana na Waandishi wa Habari Dar es Salaam na kuzungumzia kuhusu kifo cha mumewe >>>> “Kuna
habari ilitoka kwamba familia imesema ajali ya Mchungaji Mtikila ni ya
kawaida.. naipinga, aliyetoa taarifa hiyo hakuwa mwanafamilia na sio
Mwanachama wa DP… Hakuna Mwanafamilia aliyekuwa tayari kutoa taarifa
yoyote kwa niaba ya Chama wala Familia.”
“Naomba
tusaidiwe ili haki ya Marehemu ionekane ikitendeka, haya maombi
tunaomba yafike…. Tunaomba Rais aingilie kati kwa kuunda Tume huru
isiyohusisha Polisi ili kuchunguza kifo cha Mchungaji Mtikila” >>> Mama Georgia Mtikila.
Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila.
“Tunaiomba
TCRA itusaidie kumpata mtu aliyeweka picha ya Marehemu Mtikila alfajiri
siku ya ajali, kwa sababu mpaka sasahivi simu ya Mchungaji hatujui
iliko…” >>> Mama Georgia Mtikila.
0 comments:
Post a Comment