Ukiwa maeneo kama ya Mwanza au Dar es
Salaam kuna maeneo ambayo huwa zinaoneshwa movie kali kabisa na mpya
mpya.. kila Ijumaa huwa naiweka ratiba ya Movie kwa maeneo ya Mlimani City– Cinema Century, Oysterbay pamoja na Quality Center.
Kumbe kuenjoy Movie kwenye screen kubwa
wewe na watu wako sio lazima iwe kwenye Jumba kubwa la sinema, watu na
ubunifu wao wamebuni na hii mtu wangu.. mnaweza kuweka pozi lenu hata
kwenye packing ya magari na Movie ikaangaliwa kwa raha zote yani !!
Hapa ni Gili Lankanfushi kwenye Visiwa vya Maldives…
Hapo ni Hotel ya Kifahari kabisa, mnapewa na nafasi ya kuenjoy movie
kwenye eneo la kipekee, pamezungukwa na miti hivi alafu chini ni mchanga
kabisa. Kwa wapendanao, YES hapo panawafaa.
Hapo panaitwa Cinekamari, Visiwa vya Santorini Ugiriki. Usiogope
hivyo vichaka ukahisi Simba au Chui wanaweza kuibuka.. pako salama
kabisa na ni sehemu poa pia ya kuenjoy movie na watu wako wa nguvu.
Hiyo sio packing ya magari aisee !! Ni Shooting Star RV Resort, Jiji la Escalante, Utah Marekani. Jumanne,
Alhamisi na Jumamosi jioni watu wanapaki magari yao, wanacheki movie
kwenye Screen kubwa huku wamekaa ndani ya magari yao humohumo.
Raha nyingine pembeni ya Bahari, Miami Florida, Marekani.. Minazi, garden poa kabisa ya maua na mapambo mengine vimeongezea uzuri wa hapa, panaitwa Miami Beach Edition Hotel.. unakaa na watu wako mnaenjoy vizuri kabisa movie.
Kila mtu na watu wake kwenye bwawa dogodogo, mbele kuna Bonge la Screen ya Movie… Hot Tub Cinema, hizi sehemu ziko Uingereza, Marekani na Ibiza. Unakaa na watu wako kwenye bwawa dogo lenye maji ya moto alafu mnaenjoy movie na story nyingine zinaendelea.
Alamo Drafthouse kwenye
ubora wake… sahau kidogo kuhusu viti au sofa unapocheki Movie, hapa ni
mwendo wa wewe na maji ya Bwawani.. kila mtu na boya lake, mambo ya Texas Marekani mtu wangu..!!
Hollywood Forever Cemetary, Los Angeles Marekani.. unaambiwa
toka mwaka 2002 watu wa nguvu wamekuwa wakienjoy movie hapo, Bonge la
Screen na mazingira poa kabisa kwenye eneo la wazi.
Red Rocks Amphitheater, Colorado Marekani.. Jumla ya watu 16,000 wanakaa hapo kucheki Movie mtu wangu.. Hapo ni sehemu ya juu kabisa ya Milima ya Red Rocks Park, kama unakumbuka ngoma ya ‘The Storm Is Over‘ ya staa wa R&B Marekani, R. Kelly alifanyia Video yake hapo juu.
Sala Montjuic… Wenyeji wa Canada wanasema
ungekuja miaka ya nyuma hapa palikuwa giza tu na pamekaa kihasara bila
shughuli yoyote.. sasahivi mida ya jioni watu wa nguvu wanakutana
kucheki movie, hakuna kiti !! Kwa hiyo kama ukija na mkeka, godoro au
kiti kazi ni kwako !!
Soneva Kiri, hapo ni Thailand..
mambo ni kama unavyoona, Screen ya TV iko upande huu alafu watu wanakaa
upande wa pili, katikati ni bwawa la maji.. Unaweza ukashtuka kwamba
ikitokea El Nino mambo yanakuwaje hapo?? Lakini ndio hivyohivyo watu wa eneo hilo wanaenjoy Movie za Cinema Paradiso.
0 comments:
Post a Comment