Kuna Tuzo zinaitwa ANZISHA AWARDS,
nimezifahamu leo baada ya kukuta kuna majina wa Watanzania wawili ambao
wametajwa kwenye vijana 12 waliotajwa kuwania Tuzo hizo mwaka 2015.
Tuzo hizo zimeanzishwa kwa ajili ya
kuwatambua na kuwatuza Vijana wenye umri wa kati ya miaka 17 na 22 ambao
wanajihusisha na ujasiriamali na kupitia ujasiriamali wao wamesaidia
kubuni miradi ambayo inatatua baadhi ya changamoto za Kijamii.
Kwenye majina ya Vijana 12 waliotajwa kuwania Tuzo hizo wako pia Watanzania wawili, George Mtemahanji mwenye umri wa miaka 22 na Sirjeff Dennis ambaye ana miaka 21.
Vijana wote 12 hawa hapa.
Huyu ni George Mtemahanji, Mtanzania ambaye ameingia kwenye Tuzo hizo baada ya kuanzisha mradi wa umeme wa Jua na Kampuni yake inaitwa SunSweat Solar Limited, Kampuni yake inahudumia watu waishio Vijijini ambako kuna tatizo kubwa la umeme.
Mtanzania mwingine ni huyu, Sirjeff Dennis… yeye
nae yumo, Mradi alioanzisha ni wa kukabiliana na Changamoto ya ukosefu
wa Chakula pamoja na umaskini Vijijini, kupitia ufugaji wa Kuku na
Kilimo cha mbogamboga. Jamaa pia ana Kampuni yake ambayo kaipa jina la Jefren Agrifriend Solutions, Biashara yake kubwa ni kuuza Kuku na Mayai.
Fabrice Alomo, kijana wa Cameroon ambaye ameanzisha Website ya MyAConnect ambayo inasaidia Wafanyabishara wadogowadogo kuuza bidhaa kwa njia ya Mtandao.
Mabel Suglo, huyu ni kijana wa Ghana ambaye
naye ameingia kwenye list ya vijana hao 12, yeye aliguswa na nafasi ya
watu wenye ulemavu kwenye Jamii.. akaona aanzishe kitu kinaitwa Eco-Shoes Project ambapo
aliowaajiri kufanya kazi ya kutengeneza viatu ni watu wenye ulemavu…
Viatu vinatengenezwa kwa Matairi na nguo ambazo zimechakaa na hazifai
kuvaliwa.
Huyu anaitwa Farai Munjoma, kijana kutoka Zimbabwe, yeye kaanzisha Shasha Iseminar
ambayo pia ni system ya kujisomea Mtandaoni na sehemu ya mapato
anayoyapata anasaidia pia kulipia ada baadhi ya Wanafunzi ambao wazazi
wao hawana uwezo Vijijini.
Vanessa Zommi… huyu mrembo anatoka Cameroon na umri wake ni miaka 19 tu, lakini alianzisha Kampuni ya Emerald Moringa Tea, ambayo
inatengeneza majani ya Chai yanayosaidia kufanya mfumo wa Chakula
mwilini kuwa vizuri, unaambiwa majani anayotengeneza ni ya kutokana na
mmea ambao Cameroon wanauita Moringa.
Huyu ni Mnigeria, Chris Kwekowe ambaye alianzisha System ya kujisomea Mtandaoni ambayo inaitwa Slatecube na kusaidia hata wasio na uwezo wa kulipia gharama za Vyuo kujisomea Mitandaoni kwa urahisi kabisa.
Daniel Mukisa kutoka Uganda. Daniel bado ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere,
ameanzisha mradi wa Usafirishaji kwa kutumia Baiskeli, aliona kuna ishu
ya foleni na pia Barabara mbovu kwenye maeneo mengi, mradi wake
unalenga kufikisha bidhaa mpaka nyumbani kwa wateja ambao wamenunua
bidhaa kwa njia ya Mtandao, kwa baiskeli bidhaa zinawafikia wateja kwa
haraka na inasaidia pia kuokoa gharama za usafirishaji.
Chantal Butare, mrembo mwingine kutoka Rwanda ambaye alianzisha Kinazi Dairy Cooperative, mradi ambao unawasaidia Wafugaji wadogowadogo 3,200 kuuza maziwa ya ng’ombe wao. Soko la maziwa hayo liko ndani ya Rwanda na Burundi na kazi ya kuuza inasimamiwa na huyu mrembo.
Karidas Tshintsholo kutoka South Africa… nae yumo kwenye Washiriki 12 waliopita kuingia kwenye Tuzo hizo, yeye ana mradi wa Push Imsokol Clothing ambapo anajihusisha na kutengeneza T-shirt, Kofia na Masweta ambayo yana soko zuri ndani ya South Africa.
Hidaya Ibrahim kutoka Ethiopia, huyu ndiye Mwanzilishi wa Qine Association for Promoting Education Quality ambayo
inajumuisha pamoja Taasisi za Elimu Shule za Serikali na Shule Private
pamoja na Wanafunzi wao katika kutatua Changamoto za Elimu Ethiopia.
Blessing Fortune Kwomo kutoka Nigeria. Mazingira
aliyokulia yalikuwa ni magumu kiasi cha kwamba kuna wakati alikuwa
akiumwa na Familia yake ilishindwa kumudu gharama za matibabu, kwa sasa
ni Mwanafunzi wa Utabibu na ameanzisha De Rehoboths Therapeutic Studio ambayo inahudumia Majumbani baadhi ya watu wenye matatizo ya kiafya na hawana uwezo.
Hao ndio Washiriki wote kwenye Tuzo hizo
ambao wanawakilisha jumla ya Nchi tisa za Africa, Washindi watapatikana
Mwezi November 2015 ambapo zawadi itakayotolewa mwaka huu ni Dola
75,000/= kwa washindi watatu, kila mmoja Dola 25,000/= ambayo ni sawa na
Milioni 54 za Kitanzania.
0 comments:
Post a Comment